Wiki moja tangu ndege ya Malaysia iliyokuwa imewabeba
abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo bado
zinaendelea.
Mataifa kumi na mbili sasa yamejiunga pamoja
kuisaidia serikali ya Malaysia na msako huo, juhudi zenyewe zikijikita
zaidi Magharibi mwa rasi ya Malaysia.
Marekani imesema kuwa inatuma manowari zake za
kivita, pamoja na ndege maalum ya uchunguzi katika maeneo ya Bengal,
Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari hindi.
Taarifa zinasema kuwa mawasiliano hayo yanaweza
kusaidia katika kujua iliko ndege hiyo na ndio maana Marekani ikaamua
kutuma meli zake za kivita katika Bahari Hindi.
0 comments:
Chapisha Maoni