Polisi nchini Uturuki wamewazuilia wanawake wawili
waliomfanya ishara mbaya ya mkono waziri mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip
Erdogan wakati wa maandamano ya kupinga serikali.
Waziri mkuu alisikika akilalamika kuwa wanawake
wawili walimfanyia ishara inayodhihirisha utovu wa nidhamu wakati wa
maandamano na mkutano wa hadhara.
Hatua
ya kuwazuilia wanawake hao inakuja baada ya bwana Erdogan kumkaripia
mmoja wao aliyemfanyia ishara chafu ya mkono alipokuwa akielekea
kuhudhuria mkutano wa kisiasa Magharibi mwa nchi hiyo.
Waziri mkuu inasemekana alighadhabishwa mno kwa kuwa waliomfanyia ishara hiyo walikuwa wanawake wala sio wanaume.
''Ningeweza kuelewa ikiwa kitendo hiki
kilifanywa na mwanamume, lakini badala yake kimetoka kwa mwanamke , ni
vibaya sana,'' alinukuliwa akisema bwana Erdogan.
Waziri mkuu huyo amekuwa akikabiliwa na upinzani
mkali tangu kuibuka kwa kashfa ya ufisadi dhidi yake Disemba mwaka jana
ikiwahusisha washirika wake na kumsababishia changmoto kubwa katika
uongozi wake kwa miaka 12 huku uchaguzi ukitarajiwa Machi tarehe 30.
0 comments:
Chapisha Maoni