Jiji la Windhoek, Namibia |
Siku kama ya leo miaka 24 iliyopita Namibia ilipata uhuru na siku kama
hiyo huadhimishwa kama siku ya taifa. Historia ya ukoloni huko Namibia
inarejea katika karne ya 19. Wakoloni wa Kijerumani, Kiingereza na
Kireno mwishoni mwa karne ya 19 walianzisha mashindano ya kupora na
kudhibiti maliasili na utajiri wa Namibia na wakoloni wa Kijerumani
waliweza kuidhibiti nchi hiyo na kuikoloni.
0 comments:
Chapisha Maoni