Mtambo wa mawasiliano wa ndege ya Malaysia iliyotoweka wiki moja iliopita, ulizimwa kwa maksudi.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.
Alisema kuwa ndege hiyo ilibadili
mkondo na kuendelea kuruka kwa saa saba zaidi ya muda uliotakiwa
kulingana na mawasiliano yaliyorushwa kwa Satelite na mtambo wa Radar.
Ndege iliyopotea |
Bwana Razak aliongeza kwamba hatua za ndege hiyo zinaambatana na matakwa ya mtu binafsi ambaye alikuwa akiielekeza.
Nusura bwana Razak aseme kuwa ndege hiyo
ilitekwa nyara ingawa alisisitiza kwamba uchunguzi ungali unaendelea
kubaini ilikokwenda ndege hiyo.
Marubani waliokuwa wanaiongoza ndege hiyo |
Dhana kwamba ndege hiyo ilitekwa nyara ilipingwa
vikali awali lakini sasa inaonekana imerejea kuwa mojawapo ya sababu za
kutoweka kwake.
Mtambo wa mawasiliano wa ndege hiyo ulizimwa kwa maksudi na huenda marubani walifanya hivyo kwa hiari au kwa kulazimishwa.
Darubini sasa inawalenga watu waliokuwa wameabiri ndege hiyo na wafanyakazi wa ndege.
Juhudi za kuitafuta ndege ya Malaysia bado zinaendelea |
Wapelelezi watataka kujua ikiwa kumekuwa na
tukio lolote la matatizo ya kiakili, changamoto za kifamilia na
shinikizo la mawazo kwa yeyote aliyekuwa katika ndege hiyo, hasa
marubani.
Ni wiki nne tu zimepita tangu rubani wa ndege ya Ethiopia kuiteka nyara ndege akitaka kupata hifadhi nchini Switzerland.
Marubani wa ndege hiyo ya Malaysia walikuwa na rekodi nzuri tu ya kikazi ingawa polisi bado wamefanya msako nyumbani kwao.
0 comments:
Chapisha Maoni