BAADA ya minong’ono ya muda mrefu, hatimaye staa wa Bongo Fleva,
Estelina Sanga ‘Linah’ ameweka wazi kuwa anatoka kimapenzi na Nagari
Kombo.
Akiteta na kona hii, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Linah
alisema: “Ni kweli kwa sasa natoka na Kombo, ndiye mwanaume wangu, sina
haja ya kuficha. Mimi na Amini imebaki stori tu, hata yeye ana mtu
wake.”
Kombo alijipatia umaarufu siku za nyuma baada ya kuingia uwanjani na
kumkumbatia mchezaji Ricardo Kaka wa Timu ya Taifa ya Brazil iliyokuwa
ikichuana na Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni