SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa
filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo ya kushangaza, akidai kaka
yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa Kampuni ya Kanumba The Great
Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 07,2012 nyumbani
kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi, wikiendi iliyopita jijini
Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth alisema: “Kiukweli sina amani,
hii hali inanitesa sana. Kila mara ananitokea ndotoni na kunieleza mambo
yanayofanana.”
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake aliyoiacha haina mafanikio. Sasa
nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia. Analalamika kwa
nini filamu hazitolewi, ni jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo
wangu,” alisema Seth.
CHANZO: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza
ni kwamba, kila anaponitokea, lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme
kwa kasi na kutoka jasho jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na hali hiyo. Ameniuliza imenitokea
mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema lazima tufanye maombi kuondoa
hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha uso wa wasiwasi.
0 comments:
Chapisha Maoni