MREMBO aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa
Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, licha ya baadhi ya wasichana wenzake
kutokuwa na ujasiri wa kucheza na nyoka, yeye anao.
Akipiga stori na Ijumaa, Mabeto alisema awali alikuwa muoga lakini
taratibu alianza kumzoea kiumbe huyo na sasa humtumia hata katika
shughuli zake za kimodo anazofanya.
“Hizo picha nilikuwa kwenye ‘photo shooting’ (upigaji wa picha) ila
kiukweli nina utaalam wa kucheza na nyoka, unajua siyo kila mtu anao
ujasiri wa kumchezea, kwanza anatisha ila mimi nilianza kumzoea
taratibu,” alisema Mabeto.
0 comments:
Chapisha Maoni