Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za
Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini
kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya
Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda
kuangusha shoo pande hizo.
Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa
aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan
Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa
mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye
Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert
Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa
Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya
Bongo viwanja hivyo havitatosha.
“Mimi nakwambia kabisa, pale
Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa
ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders
hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa
kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna
mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya
wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu
maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’,
mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed
‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East
Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.
0 comments:
Chapisha Maoni