Jumatano, Februari 05, 2014

OLE WAKE ATAKAYE WATUMIA MAKAHABA WATOTO KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL

Wachezaji mashuhuri katika ligi za soka za Uingereza na zile za Brazil wanajiunga na kampeni ya kuwaonya mashabiki dhidi ya kuwatumia makahaba watoto wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil baadaye mwaka huu.
Wachezaji wa kilabu ya Chelsea Frank Lampard,Oscar na Ramirez wanaunga mkono kampeni hiyo inayoshirikisha kitengo cha kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza pamoja na serikali ya Brazil.
Kampeni hiyo inawaonya wafuasi wa Uingereza kwamba watakabiliwa na tisho la kushtakiwa iwapo watalipa ili kulala na wasichana walio chini ya umri 18.
Taifa la Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya milioni ya idadi makahaba watoto wanaosimamiwa na na magenge ya uhalifu na kuna hofu kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni