AMA kweli ufuska ni janga la kitaifa! Timu ya Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers, imeshafumua matukio mengi yasiyofaa kwenye
jamii lakini hili la waliobambwa ‘wakiduu’ jikoni, limetia fora, Ijumaa
Wikienda lina kisa cha ajabu.
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar
ambapo binti aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha alinaswa usiku wa
manane akifanya ngono ndani ya kibanda cha mama ntilie, sehemu ya jikoni
na kijana mmoja muuza kiti moto maarufu maeneo hayo aliyejitambulisha
kwa jina moja la Samwel.
Ikiwa kazini, OFM inayoendelea kufumua maeneo korofi kwa biashara
haramu ya ngono nchini, ilipokea taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo
zikieleza kuwa licha ya gesti zinazokumbatia biashara ya ngono na
madanguro bubu yaliyosheheni eneo hilo, kuna baadhi ya machangudoa
wamebuni staili mpya ya kwenda kwenye vibanda vya mama ntilie.
Wakiwa na ripoti hiyo mkononi, makamanda wa OFM walitinga na
‘kusavei’ maeneo yote yanayotumika kwa biashara hizo na kuweka mitego
yake ambapo ilipotimia majira ya saa 8:00 usiku ndipo iliposhuhudia
mwanamke huyo akiingia ndani ya kibanda kimojawapo akiwa na mwanaume.
Kama kawaida, OFM iliwapa dakika chache watu hao ili waanze ‘kufanya yao’.
Kama kawaida, OFM iliwapa dakika chache watu hao ili waanze ‘kufanya yao’.
Wakiwa na vifaa vyao vya kazi, OFM waliingia ndani ya kibanda hicho
na kuwakuta wawili hao wakibanjuka laivu jikoni ambapo waliwanasa na
kuwafotoa picha za kutosha huku mwanaume akiangua kilio, tofauti na
mwanamke ambaye alikuwa akiangua kicheko.
Wakizungumza na OFM kwa nyakati tofauti baada ya kutakiwa kujieleza
ilikuwaje hadi wakafanyia ngono jikoni, wawili hao walisema kuwa
walikodishiwa eneo hilo na jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Babu
ambaye huwatoza shilingi 1000/= kwa kila mwanamke anayeingia kibandani
hapo na mwanaume.
Bila kupoteza muda, OFM iliwasiliana na Polisi wa Kituo cha
Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika eneo la tukio na kuwachukua
wawili hao na kuwapeleka kituoni.
Katika hali ya kushangaza, jamaa aliyenaswa na mwanamke huyo
aliwaacha polisi midomo wazi baada ya kudai kuwa Asha alibaki na chenji
yake shilingi elfu tano aliyodai kumkabidhi kwa madai kuwa fedha hiyo
ilikuwa ni sehemu ya mtaji wake wa kitimoto.
“Jamani ninakubali kupelekwa kituoni lakini naomba Asha anipe chenji
yangu, elfu tano yenyewe nimeichukua kwenye mtaji wangu wa kitimoto,”
alisema kijana huyo.
Hata hivyo, binti huyo hakuwa tayari kurejesha chenji hivyo wote
waliishia kutupwa nyuma ya nondo katika Mahabusu ya Mabatini wakisubiri
kufikishwa kwa pilato kujibu shitaka la uzururaji.



0 comments:
Chapisha Maoni