MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher
Mtikila amekuwa burudani ya aina yake katika viwanja vya Bunge mjini
Dodoma kutokana na misimamo na misemo yake wakati akizungumza na
waandishi wa habari.
Mtikila hukusanya idadi kubwa ya waandishi kila anapozungumza huku
baadhi ya wanasiasa na wajumbe wengine wa Bunge la Katiba wakimshangaa.
Jumatatu iliyopita, Mtikila alishangaza alipodai kwamba Baba wa
Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar,
hayati mzee Abeid Amani Karume hawakuziunganisha Zanzibar na Tanganyika,
bali kitendo hicho kilifanywa na majasusi wa CIA wa Marekani, kwa ajili
ya kuhofia hali ya usalama wakati ule wa vita baridi kati ya Mataifa ya
Magharibi na iliyokuwa dola ya Urusi, USSR.
“CIA hawakutaka yatokee ya Cuba, walisema kabisa kwamba we don’t want
another Cuba in Africa (hatutaki Cuba nyingine Afrika), isipokuwa hawa
akina Nyerere walitumiwa tu,” alisema na kusababisha vicheko kutoka kwa
waandishi na wengine waliomsikia.
Kuhusu suala la posho, Mtikila alizidi kuwa burudani alipodai wao
wanastahili nyingi zaidi kwani wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini
ya Jaji Joseph Warioba walilamba fedha nyingi wakati kazi yao ilikuwa
ndogo kuliko wao watakayoifanya kwenye Bunge Maalum la Katiba.
0 comments:
Chapisha Maoni