SIMBA SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar
iliyomaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Nahodha wake, Shaaban
Nditi kuonyeshwa kadi nyekundu kipindi cha pili katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi dakika ya nane.
Mgosi alifanyiwa madhambi na beki Donald Mosoti upande wa kulia wa Uwanja, lakini akainuka na kuendelea kukimbia na mpira na refa akaridhia.
Akapiga mpira unaofanana na krosi ambao ulielekea kwenye himaya ya kipa Ivo Mapunda, lakini kwa bahati mbaya mpira ukamteleza kipa huyo na pamoja na jitihada za kutaka kuurejesha mikononi mwake, ukadondokea nyavuni.
Simba SC ilipigana kuanzia dakika ya tisa kutaka kusawazisha bao hilo, lakini hawakufanikiwa hadi zilipotimia dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic alimtoa nje kiungo Awadh Juma Issa dakika ya 36 akamuingiza mshambuliaji Ali Badu Ali na kidogo safu ya ushambuliaji ilichangamka.
Kipindi cha pili Simba SC ilicharuka na kufanya mashambulizi ya nguvu lango ni mwa Mtibwa, hatimaye kupata bao la kusawazisha dakika ya 50, mfungaji Mrundi Amisi Tambwe, aliyemalizia pasi ya Haroun Chanongo.

Mtibwa ikapata pigo dakika ya 69, baada ya Nahodha wake, Nditi kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu refa Deonisia Kyura wa Arusha.
Matokeo hayo yanaifanya Simba SC itimize pointi 31 baada ya kucheza mechi 16 na inaendelea kubaki nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City 31, Yanga SC 35 na Azam FC 36, wakati Mtibwa Sugar inatimiza pointi 22 baada ya kucheza mechi 16 pia hivyo kubaki nafasi ya tano.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Said Ndemla dk65, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’, Amri Kiemba, AMisi Tambwe, Awadh Juma/Ali Badru na Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk51. 
Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Abdallah, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Ally Shomary/Juma Mpakala dk73, Juma Luizio/Vincent Barnabas dk66 Mussa Hassan Mgosi/Abdallah Juma dk87 na Jamal Mnyate.
0 comments:
Chapisha Maoni