Kahama /Kalenga. Madiwani wawili wa Chadema kutoka Kata ya Ngokolo,
Sebastian Peter na wa Kata ya Masekelo, Zacharia Mfuko zilizopo
Shinyanga Mjini wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amekituhumu CCM kwa mchezo mchafu.
Awali CCM inadaiwa kuanza mkakati wa kuwachukua waliokuwa viongozi wa chama hicho waliofukuzwa uanachama hivi karibuni wilayani Kahama kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.

Katika mikakati hiyo, juzi kiongozi wa juu
wa Umoja wa Vijana Taifa (jina tunalo), aliingia mjini Kahama kimyakimya
na kufanya mkutano wa siri na waliokuwa viongozi hao.
Chanzo
cha habari kilidai kuwa kiongozi huyo baada ya kufika mjini Kahama
akitokea Dodoma alifikia hoteli mojawapo mjini Kahama kwa siri na
kualika baadhi ya makada wachache wa CCM ambao aliwapa masharti ya
kutotoa taarifa yoyote juu ya ujio wake Kahama. Viongozi hao
waliofukuzwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Majengo, Bobson Wambura,
Mwenyekiti wa Jimbo la Kahama, Israel Barakiel, Katibu wa jimbo hilo,
Vicent Kwilukilwa, Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo, Benedicto Shija,
Mwenyekiti Bawacha Jimbo, Kasigwa Adram pamoja na Mratibu wa Vijana
Wilaya, Vicent Manyambo.
Hata hivyo, Dk Slaa akihutubia mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Chadema, Grace Tendega alisema anatoa ruksa kwa wabunge na madiwani wasiopenda kutumikia wananchi kuondoka Chadema.
Hata hivyo, Dk Slaa akihutubia mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Chadema, Grace Tendega alisema anatoa ruksa kwa wabunge na madiwani wasiopenda kutumikia wananchi kuondoka Chadema.
0 comments:
Chapisha Maoni