ZAIDI ya kilo 200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na
kikosi cha polisi wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea
nchini Irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na
Pakistani.
Kamanda wa polisi kikosi cha wanamaji Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio
hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo
waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa
hawaijui lugha ya Kiswahili wala Kingereza na jahazi lao halikuwa na
utambulisho wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya, Godfrey Nzowa amesema
jahazi hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji
kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia
shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo
ya madawa ya kulevya aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi
huzalishwa nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni