SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba
mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu
kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa
yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu
na mahitaji.
Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo
mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake
mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na
meno kubaki nje.
Inadhaniwa kuwa wakati wa tukio hilo, baba yake mzazi alikuwa hana
akili za kawaida na inadaiwa kuwa hadi sasa bado anashikiliwa na polisi
huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukifanywa.
Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.
Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.
“Nateseka sana, inaniuma sana, baba yangu mzazi alinitafuna uso
mzima, kwa sasa sina cha kuniokoa katika maisha, fedha za kwenda India
sina japo serikali imeahidi kunipeleka, lakini natakiwa kuwa na fedha za
kujikimu kama shilingi milioni 1.8, hizo zitasaidia kupata vibali vya
kusafiria na mahitaji binafsi, naomba Watanzania waokoe maisha yangu,”
alisema Sululuka ambaye anatarajiwa kupelekwa India na serikali hivi
karibuni.
Awali taarifa za kijana huyu zilieleza kuwa alikuwa ametafunwa na
mwajiri wake lakini sasa ameamua kufunguka kwa madai kuwa aliogopa baba
yake angekamatwa na polisi.



0 comments:
Chapisha Maoni