Mahali alipokutwa kalala mtoto huyo |
Kamanda wa pilisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi |
Mtoto mwenye umri wa miezi 03
aliyefahamika kwa jina la Clara Honest amefariki dunia katika ajali ya moto
iliyotokea huko eneo la Block T majira ya saa 11:47hrs asubuhi baada ya nyumba
walimokuwa wanaishi kuungua moto.
Kipindi ajali hiyo inatokea mtoto huyo
alikuwa amelala chumbani wakati mama yake mzazi aitwaye Vailet Magava akiwa
jikoni anapika.
Katika nyumba hiyo kulikuwa na wapangaji watano, kati yao
wapangaji wawili 1. Coaster Cimon (25) mfanyakazi wa TBL na 2. Honest Martin (42)
mfanyakazi wa benki ya posta waliunguliwa vitu mbalimbali ambavyo thamani yake
bado kufahamika. Moto ulizimwa kwa ushirikiano kati ya kikosi cha zima moto na
uokoaji, jeshi la polisi na wananchi.
Chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z.
Msangi anatoa wito kwa jamii kuwa makini na kuchukua tahadhari za majanga
yatokanayo na moto kwani yana madhara makubwa katika jamii.
0 comments:
Chapisha Maoni