Jumanne, Februari 25, 2014

BARAZA ZA MITIHANI LATOA UFAFANUZI JUU YA MATOKEO YA KIDACHO CHA NNE

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya kidato cha nne yaliyotolewa wiki iliyopita, likisema kuwa ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu unapangwa kwa kuzingatia alama za ufaulu.
Ufafanuzi huo unatokana na utata uliojitokeza kwa wadau wa elimu ambao hawakuelewa vizuri kuhusu viwango vya ufaulu , alama ya chini ya ufaulu na ufaulu wa jumla wa mtahiniwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema kuwa ufaulu katika daraja la nne umezingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili.

0 comments:

Chapisha Maoni