Watu wawili wamekufa papo hapo baada ya basi la Zuberi waliokuwa
wakisafiria kutoka Mwanza na kuelekea jijini Dar-es-Salaam kumkwepa bibi
kizee mtembea kwa miguu katika kijiji cha Tumaini tarafa ya Ikungu
katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Akithibitisha kamanda wa polisi mkoani Singida SACP
Geofrey Kamwela amesema basi hilo lenye usajili wa namba T 119 AZZ
ambalo lilikuwa na abiria sitini likitokea Mwanza kupitia Singida
limepata ajali baada ya kumkwepa mtembea kwa miguu na hatimaye lika
anguka na kuserereka umbali wa mita hamsini.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa mkoa wa Singida
daktali Geogratius Banubasi amesema wamepokea maiti moja na nyingine
ikiwa njiani kupelekwa hospitalini kutoka eneo la ajali ,pia wamepokea
majeruhi arobaini ambao wengi wao wamevunjika mikono na kusababisha
kuikata na wengine wamepata majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao,
pia majeruhi wanne wanahalimbaya na wanapelekwa hospitali ya rufaa ya
KCMC mkoani Kilimanjoro.
Kwa upande wao majeruhi waliokuwemo katika basi
hilo na mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamesema walimuona bibi
kizeee Barabarani na dereva wakati anamkwepa basi lilitoka nje ya
barabara na kutereza hatimaye kuanguka
0 comments:
Chapisha Maoni