Tarehe
13.01.2014 Majira Ya Saa 04:30hrs Huko Katika Eneo La Sae, Kata Ya Mwakibete,
Tarafa Ya Iyunga, Jiji Na Mkoa Wa Mbeya Barabara Ya Mbeya/Njombe. Pikipiki
T.436 Clp Aina Ya T-Better Ikiendeshwa Na Gabriel Ngalele, Miaka 24, Kyusa,
Mkazi Wa Uyole Iligonga Kwa Nyuma Gari
T.684 Bvy Aina Ya Scania Lililokuwa Limeegeshwa Na Dereva Asiyefahamika Jina
Wala Makazi Yake Na Kusababisha Kifo Cha Mwendesha Pikipiki Huyo Pia
Kusababisha Kifo Kwa Abiria Aliyekuwa Katika Pikipiki Hiyo Ambaye Hafahamiki
Jina Wala Makazi Yake Jinsi Ya Kike.
Chanzo Cha Ajali Kinachunguzwa. Kamanda Wa
Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Z. Msangi
Anatoa Wito Kwa Madereva Kuwa Makini Wanapotumia Vyombo Vya Moto Kwa Kuzingatia
Sheria Na Alama Za Usalama Barabarani Ili Kuepuka Ajali Zinazoweza Kuepukika.



0 comments:
Chapisha Maoni