Jumatano, Januari 08, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 08.01. 2014.


WILAYA YA  CHUNYA  - WIZI WA GARI.

MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA  SAA 15:00HRS HUKO ENEO LA KUEGESHA MAGARI YA  KAMPUNI YA  SUNSHINE MINING LTD KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA MATUNDASI,  TARAFA YA  KIWANJA, WILAYA YA  CHUNYA   MKOA WA MBEYA.  MSABAHA S/O RASHID  KAFULAMA, FUNDI MKUU WA KUTENGENEZA  MAGARI WA KAMPUNI HIYO ALIIBA GARI T.421 CHG AINA YA  TOYOTA L/CRUISER SINGLE CABIN RANGI NYEUPE CHASES NO JCLB-715407036705 LENYE THAMANI YA  USD 35,000 NA KWENDA MAHALI KUSIKOJULIKANA. MBINU NI KUJARIBU KUENDESHA GARI HILO BAADA YA  KULIFANYIA MATENGENEZO.  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI   ANATOA  WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA PAMOJA NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA  MBARALI  - AJALI YA  MOTO.


MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA  SAA 20:15HRS HUKO KATIKA SHULE YA  WASICHANA YA  SEKONDARI IGUMBILO INAYOMILIKIWA NA KANISA LA LUTHERANI, ILIYOPO  KATA YA  CHIMALA, TARAFA YA  ILONGO WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. BWENI MOJA LA SHULE HIYO LILIUNGUA MOTO NA  KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA  BWENI HILO. CHANZO BADO KUFAHAMIKA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI HITILAFU YA  UMEME. HAKUNA MADHARA YA  KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI   ANATOA  WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA  MAJANGA YA  MOTO.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI
                                                           [GONGO].

MNAMO TAREHE 07.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:50HRS HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI CHA MPONZI KILICHOPO KATA YA  KAGERA, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA   MKOA WA MBEYA.    ASKARI POLISI WAKIWA DORIA /MSAKO WALIMKAMATA PRISCA D/O GODWIN, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA KAGERA    AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1.5. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI   ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



Signed by:
 [AHMED Z. MSANGI - SACP].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Chapisha Maoni