Alhamisi, Januari 30, 2014

TAARIFA KAMILI JUU YA KUFUNGIWA KWA VIDEO YA SNURA 'NIMEVURUGWA'

Inawezekana ukawa unashangaa baada ya kuona ukimya mara baada ya kutambulishwa kwa video ya Msanii Snura kisha kutoiona ikionekana mara kwa mara kwenye televisheni yako,kiu ya swali hili naikata kwa kusikiliza alichokisema Bosi anaesimamia kazi za Snura meneja wake ‘HK’.
Hk ameanza kwa kusema>>’Kilichotokea ni kwamba video ya Nimevurugwa ni video tuliyokua tunakata kiu ya mashabiki wetu waliokua wamemis vitu fulani kwenye video ya Majanga’
‘Wengi tulivyotoa video ya Majanga walizungumza mengi sana wakidai kwamba video haikuwa nzuri sana,video ya kawaida na sababu kubwa ilikua ni Snura hakukata mauno kwenye hiyo video,tukaona tukate kiu ya wapenzi wetu ambao ukiacha tu nyimbo za Snura watu wanapenda kumuona Snura akitumia maumbile yake kwenye kucheza’
‘Kwenye video ya Nimevurugwa kumekua na style tofauti sana kwenye upande wa kucheza,matokeo yake video ilipotoka siku chache vituo vya televisheni viliacha kupiga wimbo wa msanii wangu,nikiwa kama meneja nikaanza kuzunguka kujua ni sababu gani hawapigi video ya msanii wangu’
‘Baada ya kuzunguka kwenye baadhi ya vituo sababu waliniambia hawapigi kwa sababu ina viuno vingi sana na kudai vimezidi,vinashawishi ngono nilipoenda sehemu nyingine wakanambia hivyo hivyo kwamba sijui wakipiga hiyo video Tcra wanawapa barua ya onyo lakini vituo vya nje ya nchi inapigwa tu’

‘Kitu kinachonishangaza ni baadhi ya nyimbo zenye mahadhi kama ya nyimbo ya Snura zinapigwa kwenye vituo vya televisheni,nachofanya sasa hivi ni kuelekea Basata na Tcra na kuwapelekea ile nakala watuambie kama kweli ile video hairuhusiwi na ni kweli wamewakataza watu wasipige ile video,lakini mimi kama meneja sijapokea barua yoyote inayosema video ya msanii wangu imefungiwa’.
‘Hatua ya kwanza nayoifanya ni kwenda Tcra na Basata kujua kama hii kitu imefungiwa nikijua hapo nitajua kama ni kufanya upya ile video au kutoa hivyo vipande wanavyosema vinashawishi hivyo vitu,kisha nitoe upya hiyo video’.

0 comments:

Chapisha Maoni