SIKU mbili baada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa ambae pia alikuwa ni waziri wa fedha wananchi wa jimbo hilo wameipongeza serikali kwa kukarabati maeneo korofi ya barabara ya Masum
bo - Kiponzero ili kuwezesha viongozi wa kitaifa akiwemo Rais kupita bila tatizo.
Zebedayo Kalinga ambae ni mkazi wa Kiponzero alisema kuwa msiba huo na kama na ule usemi wa kufa kufahana kutokana na serikali ya mkoa kujaribu kuficha kasoro zote za miundo mbinu ya kuelekea weneo la msiba jambo ambalo wao kama wakazi wa jimbo hilo wamefurahishwa na jitihada hizo.
Hata hivyo alisema wangefurahishwa zaidi iwapo msafara wa Rais Jakaya Kikwete ungepita katika barabara ya Kalenga - Kiponzero barabara yenye miundo mbinu mibovu zaidi ili kupitia msiba huo iweze kutengenezwa kama ilivyofanyika katika barabara ya Masumbo - Kiponzero
Kwani alisema kwa siku nyingi maeneo ambao yametengenezwa yalikuwa yakisumbua watumiaji wa vyombo vya usafiri ila kwa kuwa hakuna kiongozi wa kitaifa aliyepata kufika huku suala hilo lilifumbiwa macho.
Kalinga alisema kwa upande wake mbunge wao Dr Mgimwa enzi za uhai wake amepigania kweli ujenzi wa barabara na ubovu wa barabara hiyo ila hakusikilizwa lakini baada ya kifo chake ndani ya siku mbili barabara imetengenezwa .
Hivyo alisema kama msiba huo mwili huo ungekaa nchini Afrika kusini kwa mwezi mmoja ama mwaka kulikuwa kuna uwezekano wa kijiji cha Magunga ambacho toka nchi ipate uhuru hakijapata maji safi na salama kupatiwa huduma hiyo ili kuwafurahisha viongozi wa kitaifa .
Kwa upande wake Zuwena Sanga alisema kuwa ingependeza serikali ya mkoa wa Iringa na Halmashauri ya wilaya ya Iringa katika kumuenzi mbunge huyo kusaidia kufikisha huduma ya maji na umeme katika kijiji hicho kama sehemu ya ahsante Dr Mgimwa kwa utumishi uliotukuka
Pia alishauri viongozi wa ngazi za chini kuacha kuficha matatizo ya wananchi wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuwatesa wananchi wa pembezeno ambao siku zote maisha yao ni tabu ila viongozi wa juu wanapowatembelea viongozi wa chini wamekuwa wakificha ukweli halisi wa maisha yao.
Alisema kutengeneza barabara kwa ajili ya viongozi wa kitaifa ni sawa na kuwadanganya viongozi hao ambao walipaswa kuona maisha halisi ya wananchi wao

0 comments:
Chapisha Maoni