KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amedai kuwa michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 haitafanyika mwezi
Juni na Julai kama ilivyozoeleka badala yake itafanyika majira ya baridi. Kumekuwa na mijadala mikubwa toka Qatar walipopewa uenyeji wa kuandaa michuano hiyo Desemba mwaka 2010 kutokana na hofu ya joto kali katika majira ya kiangazi katika ukanda huo ambalo linaweza kuwa hatari kwa wachezaji na mashabiki watakaohudhuria. Akihojiwa na Radio France, Valcke amesema badala ya kufanyika kipindi hicho michuano hiyo
inaweza kusogezwa mbele ya kati ya Novemba 15 na Januari 15. Valcke aliendelea kudai kuwa kama michuano hiyo ikichezwa kati ya Novemba 15 na kumalizika Desemba muda huo hali ya hewa itakuwa nzuri tofauti na Juni na Julai.
0 comments:
Chapisha Maoni