Ofisi ya Rais wa Rwanda imekadhibisha vikali uvumi ulioenea
nchini humo na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba
Rais Paul Kagame wa nchi hiyo amefariki dunia.
Taarifa zinasema kuwa, uvumi wa habari za kufariki dunia Rais Kagame,
umeamsha furaha hasa kwa wakazi wa miji ya mpaka wa nchi hiyo na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara kadhaa Rwanda imekuwa ikituhumiwa
kwa kuingilia kijeshi katika maeneo ya mpaka na Kongo.
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa taarifa na kuituhumu tena
serikali ya Kigali kwa kuyaunga mkono makundi yanayobeba silaha na hasa
waasi wa zamani wa M23 waliokuwa mashariki mwa Kongo. Hata hivyo ripoti
hiyo ya Umoja wa Mataifa imekosolewa vikali na serikali ya Rwanda.
Rais Paul Kagame mwenye umri wa miaka 56 alichukua madarakani mwaka
1994 baada ya kutokea mauaji ya kimbari yaliyopelekea watu wasiopungua
laki nane hasa wa kabila la Kitutsi kuuawa nchini humo.




0 comments:
Chapisha Maoni