STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kubembeleza penzi
kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
Ijumaa lina full mchongo.
Mnyetishaji wetu alivujisha mawasiliano
baina ya wawili hao waliowahi kuwa wapenzi kisha kumwagana ambapo
yalionyesha kuwa Nisha analitamani upya pe
nzi la staa huyo.
Mbali na mawasiliano ya ujumbe wa maandishi, chanzo hicho kilicho
karibu na mastaa hao kilikwenda mbali zaidi kwa kuvujisha picha ambazo
zilionesha Nisha akimtumia Nay huku akichombeza na meseji tofauti za
kumtega.
Baada ya kuzinasa meseji hizo ambazo chanzo kilidai
kimeziiba kutoka katika moja ya simu ya mastaa hao, paparazi wetu
aliingia mzigoni kuwasaka mastaa hao ili kujua kama wana mpango wa
kurudiana.
Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Nisha ambaye alisema: “Dah, ni kweli ninawasiliana na Nay kama rafiki wa kawaida tu.
“Nay ana demu wake na mimi nina bwana wangu.”
Kwa upande wa Nay wa Mitego alipata kigugumizi kidogo kulizungumzia hilo lakini akakiri kupata meseji hizo za mitego lakini akadai hakuna kinachoendelea kati yao.
Kwa upande wa Nay wa Mitego alipata kigugumizi kidogo kulizungumzia hilo lakini akakiri kupata meseji hizo za mitego lakini akadai hakuna kinachoendelea kati yao.
0 comments:
Chapisha Maoni