Tarehe 19.01.2014 Majira Ya Saa 11:00 jioni Huko Katika Kijiji
Na Kata Ya Itamboleo, Tarafa Ya Ilongo, Wilaya Ya Mbarali Na Mkoa Wa Mbeya, Mtoto
Lumiki Rahim, Miaka 06, Mmasai, Mwanafunzi Shule Ya Msingi Kapunga Darasa
La Kwanza Aliuawa Kwa Kupigwa Na Fimbo Kichwani Na Mtoto Bedon Said, Miaka
12, Muwanji, Mwanafunzi Shule Ya Msingi Kapunga Darasa La Sita. Chanzo Kinachunguzwa.
Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Hospitali Ya Misheni Chimala Kwa Uchunguzi Wa
Kitabibu. Mtuhumiwa Amekamatwa. Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Wazazi/Walezi
Kudumisha Malezi Bora Kwa Watoto Wao Wangali Wadogo Ili Wakue Katika Misingi Na
Ustawi Mzuri Wa Jamii Na Kujiepusha Na Vitendo Vya Uhalifu.
0 comments:
Chapisha Maoni