HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema
za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume
atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri
tena, Amani limenyetishiwa.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza
s
okoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson
lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.
JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani
alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia
nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.
“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka
mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR
akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na
kuongeza:
“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.
“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na
suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa
bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”
0 comments:
Chapisha Maoni