ZILE tambo, mbwembwe na majigambo ya Miss Tanzania 2006/07, aliye pia
msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu, zimefika mwisho kufuatia
kunyang’anywa samani za ofisi yake ya Endless Fame Film Production na
aliyekuwa mpenzi wake, Clement ‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki
mweupe, Amani limepakuliwa ikiwa imeiva.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni
kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar.
Habari za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana
na watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo
aliyomfungulia mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani
alivyomnunulia wakati wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na
ncha).
Kama njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi
kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari,
pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala
maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika
kwenye gari.
Vifaa hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video
camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa
vya kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply (ups)
pamoja na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe
kama uwanja wa mpira.
“Hali ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya
ofisi hiyo kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi
haina kitu kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
Mpashaji huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa,
chanzo cha kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema
kurejesha penzi lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Taarifa hizo zilieleza kuwa, kitendo hicho kilichochea hasira za
Clement, hasa pale Diamond alipohojiwa kuhusu kuingilia penzi hilo na
kujibu hamwogopi mtu, “ndiyo maana Clement akaamua kumwaga ugali baada
ya wawili hao (Wema na Diamond) kumwaga mboga,” kiliongeza chanzo.
Ili kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui juu ‘niuz’ hizo, mwandishi wetu
alimtafuta Wema na kukutana naye laivu juzi ambapo alikiri kukumbwa na
zahama hiyo huku akionesha mshangao wa wazi kwa kitendo alichofanyiwa na
‘zilipendwa’ wake huyo.
“Ni kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara
yangu ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu
vyote alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:
“Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”
Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”
Mwanzoni mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile
gari la kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa
halikuwa lake.Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”
Kumbe gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack Tweve.
Tweve, baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia
Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe
na kurejeshewa mlalalamikaji huyo.
Uhakika ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa
sasa jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu
wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote
yale.




0 comments:
Chapisha Maoni