Taharuki imewakumba baadhi ya wapita njia na wafanyabiashara katika
makutano ya barabara ya Morogoro na Shekilango jijini Dar es salaam,na
kusababisha baadhi ya shughuli kusimama baada ya wapita njia wawili
kuona kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono huku baadhi
ya askari polisi wakiwa na kazi ya ziada ya kuwaondoa baadhi ya wananchi
waliokuwa wakitaka kushuhudia kitu hicho.
Tukio hilo limevutia hisia za watu wengi katika
eneo hilo na kukusanyika kwa wingi wengine katika maghorofa yaliyoko
katika eneo hilo kwa lengo la kushuhudia badala ya kusimuliwa jambo
lililowafanya polisi kuzungushia kamba maalum kwa ajili ya kuwazuia raia
kufika katika eneo hilo ambapo watu wawili mtu na mwanaye ndio
walioshuhudia.
Baadhi ya askari ambao wanadhaniwa kuwa wataalam wa
mabomu kutoka katika kikosi cha kutuliza ghasia Upanga jijini Dar es
Salaam walifika katika eneo la tukio na kuanza harakati za kukichukua
kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu kwa tahadhari kubwa na baada ya
kufanikiwa kukiondoa wakakiweka katika mfuko maalum na kutoweka katika
eneo la tukio
Fichuo Tz kiguu na njia hadi kwa kamanda wa polisi mkoa
wa kipolisi wa kinondoni kwa ajili ya kupata uthibitisho kuhusu kitu
hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu na kujulishwa kuwa taarifa juu tukio
hilo inaandaliwa naa baada ya kukamilika kwake kamanda wa polisi wa
Kinondoni Camilius Wambura akaitoa taarifa hiyo.
Kamanda Wambura hakusita kutoa tahadhari kwa
wananchi pale wanapobaini kitu ambacho si cha kawaida na cha hatari kwa
maisha ya binadamu.




0 comments:
Chapisha Maoni