Jumapili, Januari 12, 2014

ACHOMWA KISU TUMBONI, UTUMBO MKUBWA WATOKA NJE, AFARIKI PAPO HAPO MBEYA

Mtu mmoja amefariki dunia jana majira ya saa tisa usiku baada ya kuchomwa kisu tumboni na utumbo mkubwa kutoka nje huko kijijini Samang’ombe, Kamsamba wilaya ya Momba mkoani Mbeya.

Taarifa kutoka kwa makachero wa polisi zinasema kuwa marehemu aliyefahamika kwa jina la Msafiri Simon, 22, Mnyamwanga, mkulima na mkazi wa kijiji cha rwatwe ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na utumbo mkubwa kutoka nje na mtu aliyefahamika kwa jina la Boidi Paschal, 36, mnyamwanga ,mkulima na mkazi wa rwatwe.
Taarifa tuliyonayo inaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa kumkuta marehemu akiwa ameketi na mkewe kilabuni.
Pamoja na hayo, Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi amethibitisha mtuhumiwa amekamatwa. Pia anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ina madhara makubwa na badala yake watumie njia za busara katika kutatua migogoro yao inayowakabili.

0 comments:

Chapisha Maoni