Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya
Linawashikilia Watu 37 Kwa Kosa La Kunywa Pombe Kabla Ya Muda. Watuhumiwa Hao
Walikamatwa Katika Matukio Matatu Tofauti Katika Jiji Na Mkoa Wa Mbeya Mnamo
Tarehe 22.01.2014.
Katika Tukio La Kwanza Sophia Bolingo
(27) Mkazi Wa Sinde Alikamatwa Na Askari Polisi Akiwa Na Wenzake 06 Katika
Kilabu Cha Pombe Kiitwacho Ngoma Nzito, Kata Ya Sinde, Tarafa Ya Sisimba Wakiwa
Wanakunywa Pombe Maeneo Hayo Kabla Ya Muda.
Kadhalika Katika Tukio La Tatu Frank
Asukile (24) Mkazi Wa Simambwe Kata Na Tarafa Ya Tembela, Wilaya Ya Mbeya
Vijijini Pia Alikamatwa Akiwa Na Wenzake 21 Wakiwa Wanakunywa Pombe Maeneo Hayo
Kabla Ya Muda. Watuhumiwa Wote Wamefikishwa Mahakamani Kwa Hatua Zaidi Za
Kisheria.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Jamii
Kuacha Tabia Ya Kunywa Pombe Katika Maeneo Tofauti Kabla Ya Muda Uliowekwa
Kisheria Kwani Kufanya Hivyo Ni Kinyume Cha Sheria Na Jeshi La Polisi Kamwe
Halitafumbia Macho Vitendo Kama Hivyo Viliendelee Kutokea. Aidha Anatoa Wito
Kwa Jamii Kutumia Muda Huo Kufanya Shughulia Mbalimbali Za Kimaendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni