Jumatano, Januari 08, 2014

22 WAPIGWA CHINI IDARA YA WANYAMA PORI

Wizara ya maliasili na utalii imewasimamisha kazi watumishi wake ishirini na mbili wa idara ya wanyama pori wanaotuhumiwa kushiriki katika vitendo vya ujangili dhidi ya wanyama pori, hujuma, pamoja na vitendo vya rushwa na hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu amesema watumishi waliosimamishwa 11 wanatoka kikosi dhidi ya ujangili Arusha, 4 pori la Akiba Rukwa-lwafi,1 kikosi dhidi ya ujangili Bunda,3 pori la Akida Maswa,1 pori la akida Selous na 1 mapori ya akida Lukwika -Lumesule Msanjesi na kuongeza kuwa wote hao uchunguzi wa kina ulifanyika na kuwabaini kuhusika na vitendo hivyo huku akisisitiza hatua kali zitachukuliwa kwa mtumishi yeyote atakayetumia wadhfa wake kuhujumu rasilimali za taifa.
Aidha ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wizara imemkamata askari wa wanyamapori mkoani Singida aliyejehusisha na vitendo vya ujangili akiwa na bunduki mbili na ndege 12 aina ya Flamingos nyumbani kwake kinyume cha sheria na tayari ameshasimamishwa kazi na hatua za kumfikisha mahakamani zinachukuliwa ili ajibu tuhuma hizo. Nao baadhi ya wananchi licha ya kupongeza hatua hiyo wamesema serikali inapaswa kutambua mtandao unaotumika ni mkubwa hivyo kuongeza jitihada zaidi kwa kutenda haki ili wale wote watakaobainiki kuhusika wawajibishwe.

0 comments:

Chapisha Maoni