Jumanne, Desemba 10, 2013

WAKULIMA WA MKONGE MUHEZA WALIA NA SERIKALI

Wakulima wa mkonge nchini wameiomba Serikali kuondoa kodi sumbufu ikiwamo ya ardhi,OSHA, kodi ya mafuta , VAT kwenye nyuzi na ushuru wa mazao ili kupunguza mzigo wa uendeshaji.
Ombi hilo lilitolewa juzi na Katibu wa Chama cha Wakulima,Wazalishaji pamoja na Wafanyabiashara wa Bidhaa za Mkonge (SAT),Raphael Ngalondwa wakati wa maadhimisho ya siku ya mkonge nchini yaliyofanyika Muheza.
Akizungumza mbele ya Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo na Mazao,,Beatus Balema alisema lengo la kutoa ombi hilolinatokana na mkusanyiko wa kodi nyingi katika sekta ya mkonge.

0 comments:

Chapisha Maoni