Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye
kashfa ya ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya
viongozi wa CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa
hiyo ilitokea mwaka 2011/12.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri
Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu
kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.
Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo zilichakachuliwa kwa
ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba mpaka sasa hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani madiwani sita
walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za kushirikiana na
watendaji katika kutafuna fedha hizo
Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na kwamba lazima
zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani.



0 comments:
Chapisha Maoni