Ijumaa, Desemba 13, 2013

HAYA NDIO YAMESEMWA NA MISS UTALII TANZANIA BAADA YA KUFUNGIWA

Miss Utalii Tanzania,shindano lenye kuhujumiwa na kuwa na maadui wengi zaidi kuliko shindano jingine lolote nchini na Afrika Mashariki na kati.
1. Tumekuwa tuki pandikiziwa washiriki mamluki kutoka mashindano mengine,kwa lengo la kutuchafua na kuchafua shindano
2. Tumekuwa tukihujumiwa na mtandao wa udhamini,ili kutukatisha tamaa na kututia hasara ili tukate tamaa
3. Tumekuwa tuki endeshewa propaganda na hila chafu kila kukicha tangu kuanzishwa kwake
4. Tumefanyiwa zaidi ya majaribio 4 na mafisadi wa sanaa na madui wa haki ya kupora hakimiliki yetu ya mashindano tangu kuanzishwa kwake
5. Uzalendo,nia na dhamira njema yetu kwa Nchi yetu na wananchi ya kubuni na kuanzisha shindano hili bila ya kuiga popote duniani,imekuwa ni kama mwiba wa mchongoma kwetu,kwani hatuja wahi kuwa na amani tangu tulipoanzisha,imekuwa ni mapambano yasiyo na kikomo,kiasi cha kutufanya tuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yetu,kiasi cha mwaka 2008/2009 kuamua kukimbilia mafichoni nyamongo kwa kuhofia usalama wetu lo!
6. Badala ya kuungwa mkono na kupongezwa tumekuwa ni gunia la majaribio ya mashambulizi na majaribio hatari ya kutuhujumu,kutupora na kuchafuana majina,utu na kuathiri fikra na uhuru wa kujitafutia ridhiki halali kwa jasho letu

0 comments:

Chapisha Maoni