Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada
ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndege kunaswa katika
uwanja wa ndege nchini Burundi.
Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.
Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na
mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shauku ya kutaka kujua
mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.
Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadam
kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania,lakini
haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa
Thailand.
Bw Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.



0 comments:
Chapisha Maoni