Afya za maelfu ya walaji wa nyama katika Jiji la Dar es Salaam
zipo hatarini baada ya kubainika kuwa nyama inayochinjwa katika
machinjio mengi haifai kwa matumizi ya binadamu.
Hali hiyo inatokana na mifugo kuchinjwa bila
kufuata taratibu za afya na kuingizwa sokoni, ikiwamo nyama hizo
kutokaguliwa na wataalamu wa mifugo kabla ya kuchinjwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika
machinjio mbalimbali ya maeneo ya Vingunguti, Ukonga, Kimara Suka,
Tegeta na Mbagala, umebaini taratibu za kuchinja hazifuatwi huku maeneo
hayo yakiwa yamejaa uchafu.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika machinjio
hayo kwa nyakati tofauti alfajiri na kushuhudia ukiukwaji wa taratibu za
uchinjaji, ambapo nyama zinatupwa ovyo, kwenye mazingira hatari, huku
nyingine zikiwekwa karibu na madimbwi ya maji machafu.




0 comments:
Chapisha Maoni