Siku kama ya leo miaka 124 iliyopita alizaliwa Jawaharlal Nehru mmoja kati ya viongozi wakubwa wa harakati ya kupigania uhuru wa India dhidi ya mkoloni Mwingereza huko Allah Abad kaskazini mwa India. Nehru alianzisha mapambano dhidi ya mkoloni Mwingereza baada ya kujiunga na harakati ya taifa ya ukombozi wa India. Jawaharlal Nehru alitiwa mbaroni mara kadhaa na kufungwa jela kutokana na mchango na nafasi yake kuu katika mapambano hayo ya kupigania uhuru wa India. Hatimaye India ilipata uhuru mwezi Agosti mwaka 1947 baada ya Mahatma Gandhi kujiunga na mapambano ya wananchi wa India na viongozi hao wawili wakubwa wa kisiasa kuongoza mapambano ya wananchi ya kupigania.
Na miaka 124 iliyopita katika siku kama ya leo Dakta Taha Hussein mwandishi na malenga mtajika wa Misri alizaliwa. Msomi huyo mashuhuri alipofuka macho akiwa mtoto, hata hivyo kipawa chake cha hali ya juu kilimuwezesha kuendelea na masomo na hadi kufikia mwaka 1918 alikuwa amekamilisha masomo yake ya shahada ya udaktari katika vyuo vikuu vya Misri na cha Sorbonne nchini Ufaransa. Dakta Taha Hussein mbali na kuwa kipofu, aliweza pia kushikilia nyadhifa za juu katika ngazi za kiutamaduni na kisayansi ndani na nje ya Misri na kipindi fulani alikuwa Waziri wa Utamaduni wa Misri.



0 comments:
Chapisha Maoni