Wanajeshi wawili wa Kulinda amani wa
Umoja wa Mataifa, wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya katika shambulizi
la kujitoa mhanga Kaskazini mwa Mali.
Raia wa kawaida pia walifariki
kwenye shambulizi lengine la bomu wakati mshambuliaji alipoingiza gari lake
lenye mabomu katika eneo la kukagua magari kabla ya kujilipua mwenyewe.
Mtoto mmoja aliuawa na mwengine
kujeruhiwa kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la Reuters likinukuu
maafisa wa serikali.
Umoja wa Mataifa una takriban
wanajeshi 6,000 nchini Mali, walioko huko kupambana na wapiganaji wa kiisilamu.
Katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon
alisema kuwa mashambulizi hayo hayataathiri kabisa lengo la UN kuunga mkono
kurejeshwa kwa utulivu na usalama pamoja na amani nchini Mali.
Baraza la usalama la UN limelaani
mashambulizi hayo kwa kauli nzito sana.
Ilielezea kusikitishwa pamoja na
kuwatakia pole jamaa na marafiki za wanajeshi waliouawa pamoja na serikali ya Mali
na Chad.
Baraza huilo limesema kuwa
waliohusika lazima watachukuliwa hatua kali na imeitaka Mali kuchunguza mauaji
hayo na kuwaadhibu waliohusika nayo.
Wizara ya ulinzi ilisema kuwa
washambuliaji wanne walihusika na mashambulizi hayo na wote walifariki.
Mwakilishi wa UN nchini Mali, Bert
Koenders, mapema mwezi huu alitoa wito wa kupelekwa kwa wanajeshi zaidi baada
ya kuongezeka kwa visa vya mashambulizi ya mabomu na makombora.
Wanajeshi wa Ufaransa, walikomboa
eneo la Kaskazini mwa Mali pamoja na miji mingine kutoka kwa wanamgambo baada
ya kuanzisha operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Jukumu la usalama hata hivyo
walilikabidhi kwa Umoja wa Mataifa mwezi Julai.



0 comments:
Chapisha Maoni