Pengo kati ya wanaume na wanawake limepungua kwa
kiasi tu katika kipindi cha mwaka mmoja. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya
kongamano la kimataifa la kiuchumi{World Economic Forum- WEF}.
Nchi za Iceland, Finland na Norway zinaongoza
orodha ya mataifa 136 ambapo kumekuwepo na usawa kati ya wanawake na
wanaume katika nyanja ya elimu, uchumi na afya.Mashariki ya kati na
Kaskazini mwa Afrika yametajwa kama maeneo ambapo hali ingali mbaya kwa
wanawake katika kupata nafasi za uwongozi, elimu na afya bora.
Nchi za Ufilipino na Nicaragua ziko kwenye kumi
bora.Kongamano la WEF limekuwa likitoa taarifa yake kwa miaka minane
sasa. Ripoti hii inajiri wakati BBC imekuwa na mwezi mmoja ulioangazia
masuala ya wanawake hususan nafasi yao katika jamii.



0 comments:
Chapisha Maoni