Askari wamesimulia mateso makali ya kutisha yaliyofanywa na magaidi
kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi juzi wakidai kuwa mateka
walikatwa viungo, macho yao kutobolewa na kutelekezwa wakiwa
wamening'inizwa katika vishikizo darini.
Watu hao walisemekana kuhanisiwa na vidole vyao kunyofolewa kwa kutumia koleo kabla ya kupofolewa macho na kunyongwa.
Watoto
walikutwa wakiwa wamekufa ndani ya majokofu ya kuhifadhia chakula huku
visu vikiwa bado vimeng'ang'ania kwenye miili yao, imedaiwa.
Wengi
wa magaidi hao walioshindwa mapigano, hatahivyo, waliripotiwa
kupatikana wakiwa 'wameteketea moto na kubaki majivu', kuchomwa moto na
mwenye msimamo mkali wa mwisho kujaribu kuficha utambulisho wao.
Taarifa
hizo za kutisha zimekuja juzi huku picha za kwanza zikiibuka kutoka
ndani ya jengo hilo lililobomoka, zikionesha rundo la miili ikiwa
imetelekezwa kila kona sakafuni.
Sehemu kubwa ya jengo hilo iliangamizwa katika mapigano kati ya magaidi na vikosi vya Kenya.
Ikiwa
imelala kwenye kifusi inahofiwa kuwa miili ya wananchi wengi wanaofikia
71 ambao wamethibitishwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya kwamba
walikuwa hawajulikani waliko.
Pamoja na wapelelezi, wakiwamo FBI
na Metropolitan Police, bado haikuwezekana kufikia sehemu iliyobomoka
ya jengo hilo kwa hofu ya kulipuka mabomu, inaweza kuchukua hadi wiki
kujua kwa uhakika nani bado yuko ndani ya jengo.
Juzi, askari na
madaktari ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuingia ndani ya
jengo hilo baada ya kuwa imedaiwa Jumanne, walizungumzia matukio ya
kutisha ndani.
"Unakuta watu wakiwa na vishikizo wakining'inia
kutoka kwenye dari," alisema mmoja wa madaktari wa Kenya, ambaye
hakutaka kutajwa jina.
"Walinyofolewa macho, masikio na pua.
Wanachukua mkono wako na kuuchonga kama penseli kisha wanakwambia
uandike jina lako kwa kutumia damu. Walicharanga visu ndani ya mwili wa
mtoto mmoja.
"Hakika kama unaangalia miili yote, isipokuwa wote
waliotoroka, vidole vimekatwa kwa koleo, pua zimenyofolewa kwa koleo.
Hapa ilikuwa maumivu."
Askari mmoja, ambaye alipiga picha kaunta
ta mikate na katika ArtCaffe, alisema alishikwa ganzi kwa kile
alichokiona hivyo anahitaji ushauri nasaha.Wataalamu wa kutegua
mabomu wakiwa na mbwa wa kutambua mabomu juzi walikuwa wakikagua
sehemu
ya jengo hilo ambayo inahofiwa kuwa na mabomu kabla ya kuruhusu maofisa
wa mahakama, polisi na vikosi kusaka miili.
Picha pia zilizoibuka
juzi zimebainisha ukweli wa kiwango cha uharibifu uliosababishwa
katikati wakati wa mapambano hayo ya siku nne kati ya vikosi vya Kenya
na wanamgambo wa Kiislamu.
Picha za kwanza zilizopigwa ndani ya
eneo hilo zinaonesha shimo kubwa katika paa la jengo hilo baada ya
ghorofa tatu kuanguka pale askari wa Kenya walipolipua bomu ndani ya
jengo, kuweza kupata nafasi ya kuwasaidia waathirika, ofisa wa serikali
alisema.
Kubomoka huko kulitokea Jumatatu pale vikosi vya
serikali vilipofanya shambulio kubwa katika jengo hilo ambako watu
wanaofikia 150 wanahofiwa kuwa wameuawa.
Wakati wa kupambana na
moto, mateka waliripotiwa kuchinjwa kuanzia sikio moja hadi jingine na
walitupwa wakipiga mayowe kutoka kibaraza cha ghorofa ya tatu huku
utekaji huo ukielekea kufika mwisho. Timu za mahakama bado zinahangaika
katikati ya milima ya vifusi, huku wakihofu miili mingine zaidi bado
haijapatikana.




0 comments:
Chapisha Maoni