Jumapili, Septemba 08, 2013

SAIDA KALORI ANUSURIKA KIFO WAKATI AKIFANYA P.A

Mwanamuziki saida kalori na mwenzake papa kishaju wamepata ajali mbaya muda mfupi ulipita katika mlima wa kashura wakati wakipita mitaani kunadi onesho lao lililotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa linas club usiku wa leo.
chanzo:Gari la wazi linalomilikiwa na kampuni ya kiroyera tours lililokuwa limewabeba limeshindwa kupanda mlima na kurudi nyuma kisha kuanguka.
wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa kagera lakini hali ya papa kishaju inaelezwa kuwa ni mbaya

UPDATE
Taarifa ambazo nimepokea kutoka kwa Bw will ruta maarufu kama Will kiroyera ambaye ndiye mmiliki wa gari lililohusika na ajali na ambaye ni mmoja wa wahusika wa shoo hiyo amenieleza kwamba Saida karoli amepata majeraha kidogo na kwamba shoo ya Usiku itaendelea kama kawaida,ila papa kishaju bado huyo hospitali ya mkoa wa kagera kwa matibabu.

0 comments:

Chapisha Maoni