Jumanne, Septemba 10, 2013

RUKWA YACHAPWA 5-1 NA TEMEKE COPA COCA-COLA

TEMEKE imejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza robo fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 10 mwaka huu) asubuhi kuizamisha Rukwa mabao 5-1.
Hadi mapumziko katika mechi hiyo ya kundi B hatua ya Fainali za Taifa iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam, washindi walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao ya washindi yalitiwa wavuni na Constantine Katepa aliyefunga dakika ya 28, Patrick Ambrose dakika ya 36 huku Hamisi Kajole akipiga mawili dakika ya 43 na 71. 
Bao la nne lilifungwa dakika ya 46 na Ramadhan Juma.

Rukwa ambayo kwa matokeo hayo imeshatolewa ilipata bao lake dakika ya 51 kupitia kwa Francisco Nkanga.
Timu nyingine katika kundi hilo ni Geita na Ilala.

Robo Fainali ya michuano hiyo itaanza keshokutwa (Septemba 12 mwaka huu).
Kila kundi linatoa timu mbili kucheza hatua hiyo katika mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola. 
Wakati huo huo: Timu za Kimondo SC ya Mbeya na Kurugenzi ya Mafinga zitatumia viwanja vya Mbozi na Mafinga kwa ajili ya mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza Jumamosi (Septemba 14 mwaka huu).
Kimondo SC sasa itatumia Uwanja wa CCM Vwava ulioko wilayani Mbozi badala ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wa jijini Mbeya.
Nayo Kurugenzi itatumia Uwanja wa Wambi ulioko Mafinga mkoani Iringa badala ya Uwanja wa Makambako ulioko mkoani Njombe.
Mechi za fungua dimba FDL msimu huu zitakuwa kati ya Burkina Faso na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, Mkamba Rangers na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, Majimaji na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Kimondo na Kurugenzi kwenye Uwanja wa CCM Vwawa katika mechi za kundi B.

Septemba 14 mwaka huu Tessema na Green Warriors zitaoneshana kazi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Siku inayofuata (Septemba 15 mwaka huu) Transit Camp na Polisi Dar (Mabatini mjini Mlandizi) wakati mechi nyingine za kundi hilo la A zitakuwa kati ya Villa Squad na African Lyon (Karume) na Ndanda FC na Friends Rangers (Nangwanda Sijaona, Mtwara). 

Kundi C ni Polisi Mara na Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT na Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United na Mwadui (Kambarage, Shinyanga) wakati Pamba na Toto Africans zitamenyana Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

0 comments:

Chapisha Maoni