Jumatano, Septemba 04, 2013

MGOMO UMEFIKIA SIKU YA PILI KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU AFRIKA YA KUSINI

Mgomo wa wafanyakazi wa migodi ya dhahabu nchini Afrika Kusini leo umeingia siku yake ya pili wakati hakuna mazungumzo zaidi yaliyopangwa kufanyika kati ya vyama vya wafanyakazi wa migodi na waajiri.
Lesiba Seshoka msemaji wa Chama cha Wafanya kazi wa Migodi cha Taifa(NUM) amesema mgomo huo unaendelea na kwamba hawakualikwa kwa mazungumzo mapya kujadili madai yao.Chama hicho cha wafanyakazi ambacho huwakilisha wafanyakazi wote wa migodi wanaogoma kimetupilia mbali ripoti kwamba imepunguza madai yao ya ongezeko la mishahara kutoka asilimia 60 hadi kuwa asilimia 10 tu.
Seshoka amesema NUM haikukubali ongezeko la mshahara la asilimia 10 na kwamba jambo hilo sio kweli,madai yao yako pale pale lakini wako tayari kwa mazungumzo ya ongezeko la mshahara kupindukia kima hicho.Waajiri wako tayari kutoaa ongezeko la mshahara la asilimia 6.5.
Maelfu ya wafanyakazi wa migodi ya dhahabu walianza mgomo jana baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya mshahara na kutishia kusababisha hasara ya mamilioni ya dola kutokana na kukosekana kwa uzalishaji katika sekta hiyo iliokumbwa na matatizo nchini Afrika Kusini.

0 comments:

Chapisha Maoni