Alhamisi, Septemba 05, 2013

MGOGORO WA ARDHI WAIKUMBA MBEYA

Wananchi wa kijiji cha Itumbi B wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameishutumu serikali kwa kuuza maeneo wanayoishi kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu bila kutoa taarifa kwa wananchi hao.
Hayo yamesemwa na wanakijiji hao ambao hawakutaka kutajwa majina kuwa wamekuwa wakishangaa kuona viongozi mbalimbali wakiingia kwenye maeneo hayo bila kuwapa taarifa zozote. 
Kwa upande wa mbunge wa jimbo Rupa, Victoria Mwambalaswa amesema hajui kama hawakupewa taarifa kuhusu kuuzwa kwa maeneo hayo na hivyo akasema ni vema mkuu wa wilaya akaelezea zaidi suala hilo. 
Naye mkuu wa wilaya ya Chunya Henry Kinawilo amesema viongozi wa kijiji walishapata taarifa za kuuzwa maeneo hayo ili yatumike na wachimbaji wa dhahabu.
Hivyo Kinawilo amesema atachukua jukumu la kufuatilia jambo hilo ili kuweza kuliweka sawa kabla mambo hayo hayajachukuwa sura mpya. 
Aidha amesema sekta ya madini kupitia ofisi ya wilaya inapaswa kuwajulisha wananchi kuhusu kuuzwa kwa maeneo ambayo serikali inataka kuwapatia wachimbaji wadogodogo.

0 comments:

Chapisha Maoni