Jumatatu, Septemba 16, 2013

KIDATO CHA TANO MWAKA HUU BADO CHENGA CHENGA

Wanafunzi waliopangiwa kusoma elimu ya kidato cha tano na sita katika shule za serikali wanafika kwa kusuasua katika shule hizo. 
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya madarasa yamekosa wanafunzi wa kutosha huku baadhi ya michepuo kadhaa ikikosa wanafunzi kabisa na mingine kupokea idadi ndogo ya wanafunzi. 
Wanafunzi wa kidato cha tano walitakiwa kuanza kufika katika shule walizopangiwa kuanzia Julai 29, mwaka huu na baadaye kuongezewa miezi mitatu, lakini kutokana na kusuasua kufika katika shule hizo, hali hiyo imeathiri mchakato wa ufundishaji katika baadhi ya shule. 
Moja ya sababu zinazotajwa kusababisha hali hiyo ni matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana ambayo yaliilazimisha serikali kuyabatilisha na kuyatangaza upya kutokana na wanafunzi takribani asilimia 60 kufeli.

0 comments:

Chapisha Maoni