Jumatano, Septemba 04, 2013

KAMA HUJUI FAIDA ZA KULALA USINGIZI WA KUTOSHA SOMA HAPA

Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi. Wanasema kuwa kulala kunasaidia katika kujenga celi mpya za ubongo. Usingizi unasaidia kuzalisha upya celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama Myelin ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi. 

Matokeo ya utafiti huu ambayo yalijitokeza katika panya wa mahabara, huenda yakachochea maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa usingizi katika kukabarabati celi za ubongo na kukuza celi mpya pamoja na kuulinda kutokana na magonjwa. 

Daktari Chiara Cirelli na wenzake kutoka chuo kikuu cha Wisconsin waligundua kuwa Panya hao walipokuwa wanalala, ndipo kemilaki hiyo ilikuwa inatengezwa kwa wingi na celi za mwili. 

Ongezeko la kemikali pia ilitegemea aina ya usingizi ambao Panya walilala hasa uliohusishwa na ndoto.

0 comments:

Chapisha Maoni