Ijumaa, Agosti 09, 2013

WAMACHINGA SASA RUKSA UBUNGO

Wafanyabiashara ndogondogo walioondolewa katika eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo wamerejeshwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika stendi hiyo mara baada ya kuondolewa ili kupisha kuhamishwa kwa kituo hicho kwenda katika eneo la Mbezi Luis jijini hapa.


Wafanyabiashara hao ambao walikua wamevunjiwa vibanda vyao na kuondolewa kwa nia ya kupisha
shughuli za kuhamisha kituo hicho,wameonekana wakianza kujenga vibanda vya muda ili kuendelea na biashara na kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za vyakula na maji.
Msemaji wa halmashauri ya Dar es Salaam,Gaston Makwembe alisema wameamua kuwarudisha wafanyabiashara hao kituoni hapo kwa muda ili huduma za maji na chakula ziendelea kupatikana katika eneo hilo huku taratibu nyingine za kuhamisha kituo hicho zikiendelea. Kituo hicho cha mabasi ya kwenda mikoani Ubungo kitahamia katika eneo la Mbezi Luis.

0 comments:

Chapisha Maoni