MASTAA wa filamu Bongo, Lucy Komba na Rose Ndauka wanadaiwa kumchunia
msanii mwenzao, Yvonne Cheryl ‘Monalisa’ kisa kikitajwa kuwa ni Prodyuza
Mghana aitwaye Prince.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai
kuwa, awali Mona na Prince walikuwa washikaji na baadaye Mona
akamtambulisha Lucy kwa jamaa huyo, hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
“Lucy alipojuana na Prince, akamchukua Rose kisha wote watatu
wakaenda Ghana eti kushuti filamu. Wakiwa huko sijui walimwaga sumu gani
na hapo ndipo uhusiano wa Mona na Prince ulipoanza kufifia.
“Mona akashangaa ila akapotezea na hata Lucy na Rose waliporudi
hawakuwa wakimchangamkia mwenzao, wakaanza kumchunia mpaka sasa,”
kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata nyeti hizo, mwandishi wetu alimtafuta Mona ambaye
alipopatikana alikiri kuwepo kwa ‘mnuno’ kutoka kwa wasanii wenzake hao,
akasema chanzo ni Prince.
“Niliamua kuachana na Prince kwa kuwa niliona ana tamaa na wasanii na
nashangaa Rose na Lucy nao wanavyonichunia, ingawa kiukweli sikupenda
kabisa kuongelea suala hili kwani sipendi shari,” alisema Mona.
Rose alipoulizwa alikuja juu na kudai hajawahi kuwa na ukaribu na Mona. Lucy hakuweza kupatikana kufungukia madai hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni