Msanii mahiri katika ulimwengu wa Bongo movie, Rose Ndauka amewawakia baadhi ya waandishi wanoandika
habari za uongo kuhusu kuripotiwa kuwa
amekutwa kaitika nyumba ya wageni akivunja amri ya sita na mwanamziki
mmoja wa muziki wa kizazi kipya.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Rose aliandika
“Dah magazeti yanapenda chokochoko kweli haswa wakimuona mtu
katulia….kama hujui uliza sio tu unaongea au unaandika kitu ambacho
ukijui……mnaudhi sana”
Huku akionesha picha ya gazeti moja la udaku lilikouwa na habari hiyo.
Hapo awali iliripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari na baadhi ya
magazeti kuwa mwanadada huyu alionekana akipapaswa ndani ya gari na
baadaye yeye na mwanamuziki huyo aliyotajwa kwa jina la dogo Nasry
kwenda kuvunja amri ya sita katika hoteli ya chumba hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni